Zulu Account ni account yenye mtaji wa dola 15,000 utainunua kwa dola 100 tu. Account hii ina leverage ya 1:100.
Ukishanunua account hii utatakiwa kukamilisha hatua zifuatazo:
1.KUFUZU HATUA YA KWANZA
Ili uweze kufuzu hatua ya kwanza unatakiwa kutumiza vigezo vifuatavyo;
- Ku-trade kwa siku zisizopungua tatu.
- Kutengeneza faida ya 8% ya mtaji uliopatiwa kwenye hii hatua.
- Kutokupata hasara inayofikia 10% ya mtaji uliopatiwa.
- Kwa siku kutokupata hasara(Daily loss) ya 5% ya balance unayoanza nayo kwenye siku.
- Usipo trade kwa miezi mitatu mfululizo itahesabika account ni dormant hivyo itafungwa
2.KUFUZU HATUA YA PILI
Utapewa upya mtaji wa dola 15,000
- Ku-trade kwa siku zisizopungua mbili.
- Kutengeneza faida ya 8% ya mtaji. Faida hii itaangaliwa baada ya wewe kufunga trades zako zote ulizofanya.
- Hasara haitakiwi kuzidi 7% ya mtaji uliopewa.
- Kwa siku kutokupata hasara (Daily loss) ya 3.5% ya balance unayoanza nayo kwenye siku.
- Usipo trade kwa miezi mitatu mfululizo itahesabika account ni dormant hivyo itafungwa.
3. HATUA YA TATU NI KUPATIWA MTAJI ULIOHITAJI.
Masharti ya mtaji huu ni kama ifuatavyo:
- Ku-trade kwa siku zisizopungua 28 bila kufanya withdrawal ya faida unayokuwa ukitengeneza.
Lakini, siku utakazofanya scalping pekee hazitahesabika kama ume trade siku hiyo. Scalping ni entry inayodumu si zaidi ya dakika moja na kutoka na pips zisizozidi tano.
- Baada ya siku 28 unaweza uka withdrawal faida yote ama sehemu ya faida uliyotengeneza.
- Utapata gawio la 80% ya faida ambayo utakua umeitengeneza Kila mara utakapo hitaji kutoa faida yako.
- Baada ya kufanya withdrawal ya faida kwa mara ya kwanza, withdrawal zinazofuata utakuwa ukifanya kwa mpishano wa siku tano kati ya withdrawal mpya na withdrawal iliyopita.
- Kutokupata hasara ya 10% ya mtaji uliopatiwa.
- Kwa siku kutokupata hasara(Daily loss) ya 5% ya balance unayoanza nayo kwenye siku.
- Malipo yako utayapata ndani ya saa moja baada ya kuwasilisha kwetu maombi ya withdrawal.